The House of Favourite Newspapers

Barnaba awakomaza Special Force Classic

0

barnaba1Barnaba

Stori: MWANDISHI WETU

Kundi la muziki linalofanya poa mkoani Tanga, Special Force Classic lipo katika hatua za mwisho za kuachia kichupa chao cha wimbo wao mpya wa Mpira wa Kona waliomshirikisha Barnaba lakini pia kwa mara ya kwanza wanatarajia kufanya shoo katika Kijiji cha Mlalo, wilayani Lushoto.

Special Force ClassicSpecial Force Classic

Akipiga stori na safu hii, kiongozi wa kundi hilo Prince Kalawa alisema kuwa, wameamua kuandaa shoo hiyo ili kuwaonesha wakazi wa eneo hilo jinsi walivyokwiva hasa baada ya kuanza kufanya kazi na msanii mkubwa Bongo, Barnaba.

“Sapoti ya Barnaba imetukomaza na kutufanya tujiamini, tuko vizuri na tumeona kwa mara ya kwanza tufanye shoo nyumbani, itakuwa ndani ya Ukumbi wa Blue Park pale Moa siku ya Idd hivyo watu waje waone burudani,” alisema Kalawa.

Leave A Reply