The House of Favourite Newspapers

BARNABA: Muziki Siyo Ajira Rasmi, Wasanii Tunatumikishwa – Video

MSANII wa Bongo Fleva, Elias Barnaba maarufu kama Barnaba Boy amesema mpaka sasa tasnia ya muziki nchini haija rasimishwa kuwa ajira rasmi hapa nchini jambo ambalo linasababisha changamoto kubwa miongoni mwa wasanii a tasnia hiyo hasa wanapotaka kufanya kazi zao nje ya nchi.

 

Barnaba amesema hayo leo Mi 17, 2019 alipokuwa akifanya mahojiano na kipindi cha Bongo 255 cha +255 GLOBAL RADIO,  na kuwapongeza Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa kazi wanayoifanya ya  kusimamia tasnia hiyo kwa weredi na kuwahimiza wasanii kufuata maadili.

“Siwalaumu sana BASATA wala COSOTA kwa sababu wanasimamia misingi ya tasnia, wamekuwa wakisimamia sanaa vizuri, huwezi kumridhisha kila mtu, bado ninaamaini Serikali ina nguvu ya kutusemea na kutupigania. Mpaka sasa muziki bado haujarasimishwa kuwa ajira rasmi, lakini sisi bado tunatumikishwa vitu kama rasmi, tunalazimika kulipishwa kodi tukienda kwenye matamasha, huwezi kufanya shoo bila vibali.

 

“Juzi nimenyimwa viza ya kwenda Marekani kwenye shoo, na moja ya vigezo ilikonekana kama muziki siyo sababu kubwa ya kupewa kipaombele cha kuingia nchini humo, BASATA walinisaidia lakini ndo hivyo, ilibidi niahirishe shoo. BASATA wanasaidia sana lakini wapo wasanii wachache wanaihujumu hasa wakiwa na matatizo,” alisema Barnaba.

 

Mbali na kutambulisha Albamu yake mpya ya Gold ynye nyimbo 10 na kazi zake alizotoa akishirikiana na wasanii wa ndani akiwemo Rapa G Nako na wengine wa nje ya Bongo, Barnaba pia amewatambulisha wasanii wake wapya akiwemo Mulla Flavour ambao anashirikiana nao katika Lebo yake Barnaba Boy Classic.

MSIKIE BARNABA AKIFUNGUKA

Comments are closed.