Baraza la Usalama Ukraine Lafanya Umafia, Lakamata Benki 2 za Urusi

Benki ya Kimataifa ya Hifadhi (MR Bank) inayomilikiwa na Sberbank ya Urusi

MAMLAKA mjini Kiev nchini Ukraine imekamata mali za benki kuu mbili za Urusi nchini humo ambazo ni Sberbank na VEB.RF.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, uamuzi huo umechapishwa kwenye Tovuti ya Baraza Kuu la Ukraine jana Alhamisi Mei 12, 2022.

Prominvestbank (PIB) inayomilikiwa na Shirika la Serikali la Urusi VEB.RF

Kulingana na uamuzi wa Baraza la Usalama na Ulinzi la Kitaifa la Ukraine wa Mei 11, 2022 na kuidhinishwa siku hiyohiyo na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy umeeleza kuwa Kiev itatoa asilimia 99.8 ya hisa za Prominvestbank (PIB) inayomilikiwa na Shirika la Serikali la Urusi VEB.RF na asilimia 100 ya hisa za Benki ya Kimataifa ya Hifadhi (MR Bank) inayomilikiwa na Sberbank ya Urusi.

 706
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment