The House of Favourite Newspapers

BASATA KUTETA NA NAY WA MITEGO

Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) linatarajia kuku-tana na staa wa Bongo Fleva, Emm-anuel Elibariki ‘Nay’ ili kuteta naye kuhusu mustakabali wa kazi zake.

 

Oktoba 17, mwaka huu Basata ilimuita Nay na kumpatia barua yenye ukarasa mmoja iliyokuwa ikielezea ajenda ya kukutana naye kuwa ni kujadili mwenendo ya kazi zake.

 

Nay alikaa kimya kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kufungiwa kazi yake na Basata na kuamua kurudi kwa kuachia Ngoma ya Alisema.

 

Akizungumza na Over Ze Weekend kuhusiana na taarifa ya kuitwa Basata, Nay alisema: “Ni kweli nimepokea barua na nitatekeleza wito.

 

“Waliniita Basata na nilipokwenda ndiyo nikapatiwa barua yenye ukurasa mmoja na nilipoifungua ndani kuisoma ndiyo nikakutana na maelezo ya kutakiwa kufika Basata Jumanne (kesho) ambapo tutakaa meza moja na uongozi wa Basata kujadili mwendendo na mstakabali wa kazi zangu za kimu-ziki.”

Rommy Jones, Mlela, Hemedy walivyotoa Msaada

Comments are closed.