The House of Favourite Newspapers

Basata Walinirudisha Sana Nyuma

0

 

NA BONIPHACE NGUMIJE |GAZETI LA UWAZI| SHOWBIZ

MKALI wa mich­ano ambaye anakim­biza kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva kwa sasa na Wimbo wa Wapo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amefunguka kuwa miongoni mwa vitu vilivyomrudisha nyuma kimuziki asiwe mbali zaidi ya hapo alipo ni kufungiwa kwa baadhi ya nyimbo zake pamoja na yeye mwenyewe na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).

Akichonga na Uwazi Showbiz, wikendi hii Nay alifunguka kuwa Basata walimjeruhi zaidi walipoufungia wimbo wake wa Pale Kati Patamu maana walisababisha akakosa dili la ubalozi alilo­takiwa kulipwa shilingi milioni 50, lakini pia takriban shilingi milioni 30 alizotumia kuandaa video ya wimbo huo hazikurudi.

“Kiukweli Basata sometimes wananije­ruhi sana wanavyokuwa wanazifungia ny­imbo zangu, unajua Basata wanatak­iwa kuelewa kuwa mimi ninapokuwa nimeach­ia wimbo mpya watu wengi wanatamani kuusikia, sasa wanaposikia na kuanza kujadili mambo mengi yanasemwa, wasisiki­lize hayo, wenyewe wasi­mame katika misingi ya kazi yao tu basi hapo wataonekana watendaji wazuri zaidi,” alisema Nay.

Leave A Reply