The House of Favourite Newspapers

BASATA Yaufungia Wimbo wa Mwanza wa Rayvanny, Diamond – VIDEO

BARAZA la Sanaa Tanzania (Basata) leo Jumatatu, Novemba 12,2018, limetangaza kuufungia wimbo mpya wa mwanamuziki Rayvanny kwa maelezo kuwa unahamasisha masuala yaliyo kinyume na maadili ya jamii na kwamba usipigwe wala kuchezwa mahali popote.

 

Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mungereza,  amesema wanafanya mawasiliano na mamlaka nyingine ili kuchukua hatua zaidi kwa kuwa tayari wimbo umeenea mitandaoni na kuongeza kwamba iwapo wataupiga katika tamasha lao la Wasafi linalotarajiwa kuanza Novemba 24, 2018 nalo watalifungia.

 

“Tumesikitishwa sana na msanii mkubwa kama Diamond kushiriki kuimba wimbo usio na maadili kwa kuwa ni msanii mkubwa anayetazamwa kama kioo na jamii. Maneno yaliyotumika katika wimbo huo yanahamasisha ngono kinyume na maumbile na matusi mengine yanayobomoa maadili.

 

“Nimesikitishwa sana na maneno yaliyotumika, hivi wanavyoimba hivyo hawaoni kama ndugu zao wanaweza kusikiliza wimbo huo? Maana kutamka hadharani ni sawa na kuongea mbele ya mama yake au watoto wake,” alisema Mungereza.

BASATA – “WCB ni wap….v, Diamond Anahamasisha Ushoga”

Comments are closed.