Bashungwa Ampongeza Rais Samia kwa Fursa ya Kutumikia Watanzania

Mbunge na aliyekuwa Waziri, Innocent Bashungwa, ameandika ujumbe wa shukrani kwa Mwenyezi Mungu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na wananchi wa Jimbo la Karagwe, kwa fursa na ushirikiano waliompa katika kipindi chake cha utumishi wa umma.
Katika ujumbe huo, Bashungwa amesema:
“Naomba kumshukuru Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fursa adimu uliyonipa katika vipindi mbalimbali kuwatumikia Watanzania. Naomba nikuahidi tutaendelea kuunga mkono juhudi na maono mazuri ya uongozi wako pamoja na Serikali ya Awamu ya 6 unayoiongoza.”
Mbunge huyo pia amepongeza wananchi wa Jimbo la Karagwe kwa ushirikiano na imani waliyoonyesha kwake, na kuahidi kutumia muda wake mpya wa ziada kufanikisha kazi za maendeleo jimboni kwa kasi zaidi.
Ujumbe wake umehitimishwa kwa kauli ya motisha:
“Kazi na Utu, Tunasonga Mbele.”
Bashungwa amesisitiza dhamira yake ya kuendelea kuhudumia wananchi na kuunga mkono sera na maono ya Serikali ya Awamu ya 6.

