The House of Favourite Newspapers

Magari 4 Yagongana, Basi la Lateketea na Kuua

0

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisaha malori matatu mkoani Songwe.
Ajali hiyo iliyotokea wilayani Mbozi katika mji wa Mlowo imehusisha basi la Classic lenye namba za usajili 68842 AK 05 linalofanya safari kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambalo limeteketea kwa moto baada ya kuligonga lori lililokuwa limeegeshwa barabarani baada ya kupata hitilafu.

 

Kwa mujibu wa taarifa ya awali iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa Songwe, Omary Mgumba amesema basi hilo lilikuwa na abiria 13 na wahudumu sita.
Mgumba amefafanua kuwa, chanzo cha ajali ni madereva wa malori mawili, moja lililokuwa limebeba mahindi likitokea njia ya Tunduma na jengine lililokuwa limebeba mbao likitokea njia ya Dar es Salaam kushindwa kuliona lori lililokuwa limeegeshwa hivyo dereva wa basi la Clasicc alipojaribu kulikwepa lori la mahindi akaligonga lori lilokuwa limeegeshwa na basi hilo kuanza kuwaka moto.

Mkuu wa Mkoa amesema majeruhi 18 wamepelekwa katika hospitali ya mkoa wa Songwe na wawili kati yao wamehamishiwa hospitali ya rufaa ya Mbeya kutokana na hali zao kuwa mbaya. Mgumba ameongeza kuwa kati ya majeruhi hao, wanane ni raia wa Tanzania na 12 ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Leave A Reply