Breaking News: Basi la Abood Lateketea kwa Moto Chalinze – Video

BASI la abiria, mali ya Kampuni ya Abood, lenye namba za usajili T 877 DJP linayofanya safari zake kati ya Morogoro na Dar es Salaam,  limeteketea kwa moto karibu na eneo la Mzani wa Vigwaza, Chalinze mkoani Pwani leo Jumanne, Februari 12, 2019.

Chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa kuwa ni hitilafu katika mfumo wa umeme wa gari hilo, ambapo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, amesema hakuna madhara yaliyotokea kwa binadamu ambapo watu wote wametoka salama, pakiwa hakuna aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa.

Toa comment