AJALI mbaya imetokea mapema leo Jumatano, Aprili 15, 2020, baada ya basi la abiria mali ya Kampuni ya Kamwana’s Express aina ya Scania Marcopolo kuteketea kwa moto katika eneo la Bwawani nje kidogo ya Mji wa Morogoro huku chanzo cha moto huo kikiwa hakijajulikana.
Basi hilo likiwa na abiria lilikuwa likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea jijini Dodoma, lakini hakuna abiria aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa.
Tutaendelea kukujuza taarifa zaidi kuhusu tukio hilo, kaa karibu na mitandao ya Global Publishers.


