Basi la Rungwe Lapata Ajali Morogoro na Kuua Watatu

Watu watatu wamefariki na 16 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la Rungwe Express na gari jingine maeneo ya Iyovi mkoani Morogoro, jana Alhamisi, Novemba 29, 2018.

Basi hilo la Rungwe Express linalofanya safari kati ya Mbeya na Dar es Salaam liligongana na gari hilo  dogo la abiria linalofanya safari kati ya Iringa na Morogoro.

Kamanda wa Polisi Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema uchunguzi unaendelea kujua chanzo.

Loading...

Toa comment