5 Wajeruhiwa Basi ‘Simba Mtoto’ Likipata Ajali Chamwino- Video

WATU watano wamejeruhiwa wakati basi la abiria kampuni ya Simba Mtoto linalofanya safari zake kati ya Dodoma na Tanga kupata ajali  majira ya saa 12 alfajiri katika Kijiji cha Chinangali, Kata ya Buigiri, Wilaya ya Chamwino baada ya kugongana na lori la mizigo.

 

Kwa mujibu wa mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo aliyefahamika kwa jina la Michael ambaye pia ni mwanachama wa Chama cha Msalaba Mwekundu Mkoani Dodoma aliyekuwa akimsafirisha mdogo wake kutoka Dodoma kwenda shuleni Tanga, akizungumza na Global Publishers, amesema:

“Taarifa nilipata mapema kwa kuwa mimi pia ni nilikuwa nikimsafirisha mdogo wangu anayerejea shule kuendelea na masomo yake mkoani Tanga, yeye alipandia njiani maeneo ya Njiapanda ya Chamwino ambapo kuna kituo cha abiria.

 

“Baada ya kupewa taarifa ya ajali nilifika eneo la tukio haraka na kuwapigia simu wanachama wenzangu waliopo katika kata yangu ili kutoa msaada wa huduma ya kwanza kwa majeruhi.

“Tulikuta majeruhi watano lakini hakukuwa na kifo, tuliwapa taarifa uongozi wa mkoa ambao walifika haraka wakiongozwa na Mratibu wa Chama cha Msalaba Mwekundu Mkoani Dodoma, Michael Mshingo  wakiambatana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa. Haraka tuliwanasua majeruhi wote na kuwakimbiza  hospitali.

 

“Ninamshukuru Mungu, mdogo wangu amepata majeraha madogo  kichwani, kuchubuka shavuni, mikononi na mgongoni lakini kwa sasa amepelekwa hospitali kwa matibabu zaidi,” amesema shuhuda huyo.Tecno


Toa comment