Basi Lapinduka Mbeya, Watu 22 Wajeruhiwa

BASI la abiria lenye namba ya usajili T.629 CQC Scania lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Mwanza limeacha njia na kupinduka kisha kusababisha majeruhi na uharibifu wa gari hilo na baadhi ya mali za abiria, leo Septemba 10, 2020 Katika maeneo ya Inyala – Mablock, Kata ya Inyala Mkoani Mbeya,  Barabara kuu ya Mbeya – Njombe huku chanzo kikiwa ni mwendokasi wa dereva.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema abiria 22 wamepata majeraha sehemu mbalimbali kati yao 12 ni wanaume na 10 ni wanawake na kwamba baadhi yao wamevunjika miguu.

 

Amesema majeruhi wanane kati yao wanaume watano na wanawake watatu wamepelekwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya na wengine 14 kati yao saba ni wanaume na saba ni wanawake wanaendelea kupatiwa matibabu Kituo cha Afya Inyala lakini.

Toa comment