The House of Favourite Newspapers

BATA LA MAMA DIAMOND… NANI ANATESEKA?

UKISIKIA vijana wa kileo wanasema ‘kula bata’ hawamaanishi kula nyama ya mfugo bali ni kufanya starehe; yaani kutua shida zote chini na kuigeuza dunia kama peponi. 

 

Juzi kati bata la mama mzazi wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim liligeuka gumzo mitandaoni baada ya picha za tukio kuonekana laivu na kuufanya msemo wa Nani Anateseka kuwahusu wengi.

 

PICHA KAMILI LIKO HIVI

Mwishoni mwa wiki iliyopita mama Daimond kupitia ukurasa wake wa Instagram alirusha picha za pozi mbalimbali akiwa anaogelea kwenye bwawa akiwa na mumewe aitwaye Maisala Shamte. Muonekano wa picha ni kama unavyoonekana kwenye ukurasa wa mbele ambapo wale wenye kuteseka na ya wenzao walipoziona waliunda vikosi vya kumshambulia mama Diamond kwa lugha za kuudhi.

MAMA DIAMOND AAMBIWA ANAJIAIBISHA

Si vyema kuzirejea komenti hizo kwenye gazeti hili lakini nyingi zilikuwa na maudhui ya kwamba kitendo cha mama huyo kupiga na kuposti picha za aina hiyo ni kujiaibisha. Kikubwa ambacho kilimponza mama huyo wa msanii ni umri wake kwamba eti haustahili kufanya mambo  hayo ya vijana na kwamba angekubali kuacha mambo ya ujana na kujiheshimu kama mtu mzima mwenye wajukuu.

MAMBO YA DINI YAIBULIWA

Pamoja na watu wengine kuwatetea Sanura na Shamte kwamba walichokifanya hakikuwa na shida, wenye dini zao waliibuka na kusema: “Ni haramu kabisa mtoto wa Kiislamu kuonesha sehemu zake nyeti hadharani.

 

“Utupu wa mwanamke kwa mujibu ya maandiko unaanzia kwenye mwisho wa vitanga vya mikono na miguu. “Sasa kuanika mapaja nje kwa mwanamke wa kiislamu ni sawa na kutembea utupu barabarani labda kama huyo mama Diamond awe si muislamu,” alisema shehe mmoja wa msikiti uliopo Kijitonyama alipoulizwa na mwandishi wetu kuhusu ubaya wa picha hizo.

MAJIBU YA WAHUSIKA

Baada ya kuona kama kuna wanaoteseka na tukio hilo la watu wazima tena mtu na mkewe kujiachia na vinguo vifupi na kutupia picha mitandaoni, Risasi Mchanganyiko liliona isiwe shida, wahusika watafutwe ili wajibu hoja. Alipopigiwa simu mama Diamond hakupokea lakini Shamte alipatikana na kufunguka yafuatayo:

 

“Mimi sioni tatizo, naona ni kawaida tu kwani tulikuwa nyumbani kwetu tunaogelea kama watu wengine wanavyofanya.” Majibu hayo yawafikie wote wanaoteseka na picha hizo kwamba hakuna tatizo lolote na hasa ikizingatiwa kwamba uzee siku hizi mwisho Chalinze, Dar hata mama Diamond ni bebi tu.

ESMA AFURAHIA BATA LA WAZAZI WAKE

Katika kuonesha kwamba familia ya mama Diamond haikuona shida ya bata walilokula wazazi wao mdogo wa Diamond Esma Khan alizifuata picha hizo kwenye ukurasa wa mama yake na kuandika: “Nawaonea wivu.”

 

FAMILIA YA DIAMOND KAMA WAZUNGU

Mara nyingi familia ya Diamond imekuwa ‘ikijiachia’ sehemu mbalimbali kwa staili za maisha ya kizungu ambapo mambo ya mama na mwana kubusiana yamekuwa siyo kitu kigeni. Maisha ya mama, baba na watoto kuchangamana bila kuwa na mipaka mikubwa ni staili za wazungu ambapo Kibongo imekuwa ikichukuliwa kuwa ni kitu cha ajabu.

Comments are closed.