Bavicha: Hatuogopi Kufa, Jaribuni Kuifuta Chadema Muone! – Video
Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA), Patrick Ole sosopi, amezungumza na waandishi wa habari leo Machi 31 katika makao makuu ya chama yaiyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam akidai wanaifahamu mikakati inayopangwa juu ya kukifuta chama hicho.
Ole Sosopi amesema wameshavumilia vya kutosha, huku wakitoa onyo na kubainisha kuwa wapo tayari kwa lolote hata kama litagharimu maisha yao.
Aidha, amezungumzia kesi inayowakabili viongozi wa juu wa chama hicho ambao hivi sasa wapo rumande, akiwemo Mwenyekiti wao Freeman Mbowe na viongozi wengine watano waandamizi ambao ni, Katibu Mkuu Vicebt Mashinji, Peter Msigwa, John Mnyika, Ester Matiko na Salum Mwalimu.


Comments are closed.