The House of Favourite Newspapers

Beka Atoboa Sababu za Kuisusa Bongo Fleva

Beka Ibrozama.

“WEWE ndiyo nyota yangu kama TID, nikikuudhi usinikimbie kama Amini, natumaini utanielewa zaidi ya yule Becka, nikikuudhi nitakubembeleza kama Barnaba Boy, usininyweshe sumu ya mapenzi usiwe mama mubaya, mimi siyo mgeni wa mapenzi maumivu nayajua, siyo kisa pombepombe iliyonifanya niropoke, siyo kisa pombepombe iliyonifanya niropoke, oooh, daima na milele min’takuwa nawe maisha yangu yote kama Marlow…”

Hiyo ni mistari mitamu kutoka kwenye ngoma iitwayo Natumaini ya mwanamuziki ambaye si mwingine bali ni Beka Ibramozama.

 

Huyu ni mwanamuziki mkali aliyekuwa anafanya vyema kwenye tasnia ya muziki Bongo wakati alipokuwa kwenye Jumba la Kukuza Vipaji Tanzania (THT), lakini baada ya kutoka hapo alipoteza ile nguvu ambayo alikuwa nayo kwenye muziki na kupotea.

Kwa muda mrefu Beka, amekuwa akijaribu kufurukuta kuweza kurudi kule ambako alikuwa, lakini kiukweli hakuweza kufanikiwa ingawa aliweza kutoa ngoma kadhaa zikiwemo Narudi Kazini pamoja na ‘cover’ ya wimbo wa Hero wa mwanamuziki Adele.

 

Lakini pia kuna kipindi Beka aliibuka na kusema kwamba anahitaji kurudi upya kwenye gemu na kivingine ambapo atakuja na bendi. Ni zaidi ya mwaka tangu aseme hivyo, lakini bado hajaweza kupata  ‘kavareji’ kihivyo kwenye media.

Sasa Risasi Mchan-ganyiko limeamua kumta-futa ili aweze kueleza kwa nini ame-po-tea, changamoto zake za kimuziki.

 

Risasi: Becka mambo vipi?

Beka: Poa, kazikazi tu!

Risasi: Ni kweli, lakini hatuzisikii hizo kazi nini kinae-ndelea?

Beka: Kwa mwaka huu mipango ni mikubwa sana kwa maana

ninatarajia kutoa ngoma nne, mbili za bendi na mbili zangu mwenyewe.

Risasi: Tukizungumzia bendi, muda mrefu umesema utatoka na bendi, kwa hiyo tayari inafanya kazi na inapiga muziki wapi?

Beka: Bendi inafanya kazi muda sasa mbona! Inaitwa Spidoch Music Band, niliizindua mwaka jana kwenye Ukumbi wa Next Door na kila Jumatano tunapiga kwenye ukumbi wa Set Jet Lumo.

 

Risasi: Kwa hiyo kwa sasa kazi zako nyingi zitakuwa zinasimama na bendi na vipi huko kuna changamoto gani?

Beka: Ndiyo, kazi zangu nyingi zitakuwa pamoja na bendi. Lakini pia nitakuwa ninafanya kazi zangu peke yangu. Kuhusu changamoto zipo nyingi na siku zote kwenye gemu hazikosekani. Kikubwa ukiwa fundi lazima utafahamu namna ya kukabiliana nazo.

Risasi: Lakini ulipotea kabisa na ukawa husikii na umelisusa gemu, bila shaka miongoni mwa vitu vilivyokupoteza ni changamoto, je kwa sasa umejipanga vipi kukabiliana nazo?

 

Beka: Kilichonipoteza na kulisusa gemu kiukweli ilikuwa hasa ni maandalizi ya bendi yangu. Nilihitaji kutengeneza kitu ambacho kitanifaa mpaka uzeeni. Wasanii walifanya vizuri na maisha yao ni mabovu? Sasa nisipojifunza kutoka kwao kesho nitakuwa wapi? Ndiyo maana niliamua kurudi nyuma kidogo ili niweze kutengeneza kitu ambacho kitanifaa kwenye maisha yangu leo na kesho.

Risasi: Kuna kipindi pia katika harakati zako za kurudi uliwahi kutoka na projekti ya kuimba nyimbo za makabila tofauti, kwa sasa hiyo projekti imeishia wapi?

 

Beka: Inaendelea na kiukweli niliimaliza. Kikubwa watu wanaokuja kwenye shoo za bendi yangu wanapata vitu vingi ikiwa kusikiliza ngoma za makabila yao.

Risasi: Mpaka sasa wewe na bendi yako mmefanya kazi gani ambazo zinasikika hewani?

Beka: Zipo nyingi kiukweli. Miongoni mwake ni Mzazi Mwenzangu na Come Back.

Risasi: Kuna tofauti gani kufanya kazi solo na kufanya na bendi?

 

Beka: Kazi na bendi unakuwa siriasi sana kwa sababu kuna watu pia wanakuangalia tofauti na kuwa solo kila kitu unafanya kwa ajili yako mwenyewe.

Risasi: Ni mwanamuziki gani wa Bongo Fleva kwa sasa unayemkubali?

Beka: Ninamkubali zaidi Nandy.

Risasi: Unawaambia nini mashabiki wako?

Beka: Wategemee mambo makubwa kwa sababu mimi na bendi yangu nimejipanga vilivyo

Comments are closed.