Beka: Mimi ni Msanii wa Kwanza Kumuimbia Magufuli

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva anayefanya poa na ngoma ya Hapa Kazi tu, Bakari Katuti ‘Beka Flevour, amefunguka kuwa yeye ndiye msanii wa kwanza kumuimbia Rais John Magufuli.

 

Akizungumza na AMANI, Beka amesema kuwa hajaimba wimbo wa ‘Hapa Kazi tu’ kwa ajili ya kampeni, bali ni kwa kumpongeza rais Magufuli.

“Naweza kusema mimi sikuimba kwa ajili ya kampeni, bali ni kwa kumpongeza mheshimiwa Rais Magufuli. Mimi ndiye mtu wa kwanza kubadili wimbo wangu na kumuimbia rais, nilikaa nao ndani kwa sababu nilitaja chama na mashabiki wengine hawapendi mambo ya chama,’’ alisema Beka Flevour.

Stori: Happyness Masunga

Toa comment