The House of Favourite Newspapers

Beki Mpya Mghana Aandaliwa Mkataba Simba

Beki mpya Mghana, Lamine Moro.

AKICHEZA mechi yake ya kwanza akiwa na Simba, beki mpya Mghana, Lamine Moro inadaiwa amemkosha Kocha Mkuu wa timu hiyo Mbelgiji, Patrick Aussems huku akitamka haoni sababu ya kumuacha nyota huyo katika usajili wake wa Caf.

 

Simba, tayari imeshusha wachezaji watatu kwa ajili ya kujaribiwa kabla ya ku­wasajili katika usajili wa Caf ili kukiimarisha kikosi chao katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Wachezaji hao waliotua nchini ni Mtogo, Hunlede Abel, Sadney Urikhob raia wa Namibia na Moro am­baye yeye tayari ameku­balika na Aussems baada ya kuonyesha kiwango kikubwa.

 

Akizungumza na Cham­pioni Ijumaa, Aussems alisema amefurahishwa na kiwango cha beki huyo kwa dakika alizomuona akiwa uwanjani akicheza mchezo wa robo fainali ya Sport­Pesa Cup walipocheza na AFC Leopards ya Kenya.

 

Aussems alisema wakati beki huyo akiendelea na majaribio hayo, anahi­taji muda wa kuendelea kumuangalia mazoezini na kwenye mchezo wa leo watakapokuwa uwan­jani wakicheza mchezo wa nusu fainali na Bandari ya Kenya.

 

“Nimeangalia upigaji wake wa pasi, ukokotaji wake mpira na ukabaji katika kuokoa na ku­zuia mashambulizi yupo vizuri Moro, lakini ninahi­taji muda wa kumuangalia vizuri.

 

“Nitamuangalia katika mazoezi yangu ya kila siku na katika mchezo wetu wa nusu fainali tutakaocheza na Bandari, lakini katika mchezo wetu na Leopards alicheza vizuri.

 

“Lakini kwa upande wa huyu mshambuliaji mpya aliyekuja naye kwenye ma­jaribio ambaye ni Hunlede (Abel), yeye bado hajani­furahisha kiwango chake kwa dakika alizocheza,” alisema Aussems.

Comments are closed.