Kartra

Beki Simba SC Atua Ghana

KLABU ya Medeama inayoshiriki Ligi Kuu ya Ghana, imethibitisha kukamilisha usajili wa beki wa zamani wa Simba raia wa Ivory Coast, Zana Coulibally.

 

Beki huyo anayecheza upande wa kulia, amesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili akiwa mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba ndani ya Klabu ya AS Vita ya DR Congo mwishoni mwa msimu uliopita aliyojiunga nayo baada ya kuondoka Simba.

 

Taarifa rasmi ya Klabu ya Medeama, ilieleza kwamba: “Medeama inayo furaha ku-tangaza kukamilisha usajili wa beki wa kulia raia wa Ivory Coast, Coulibaly Zana Oumar kwa mkataba wa miaka miwili.

 

“Coulibaly amewahi kupita katika klabu za Africa Sports, ASEC Mimosas na timu yenye nguvu kutoka Tanzania, Simba SC, ambapo akiwa na Simba nyota huyu mwenye miaka 27 alikuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kilichot-waa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2018/19.”

 

Mbali na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, beki huyo alikuwa kwenye kikosi cha Simba kilichofika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2018/19.

 

Katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huo, beki huyo alikuwa akipata nafasi ya kucheza upande wa kulia wakati ambao Shomary Kapombe akiwa majeruhi na kuonesha uwezo mkubwa.

STORI NA JOEL THOMAS, Dar es Salaam


Toa comment