The House of Favourite Newspapers

Beki Simba SC, Yanga SC Achunguzwa na Fifa

Beki wa zamani wa Simba, George Uwino.

 

SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (Fifa), limeanza uchunguzi makini dhidi ya beki wa zamani wa Simba, George Uwino ambaye inasemekana alilipwa mamilioni ya shilingi ili kuuza mechi za timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars.

 

Katika ripoti ya awali yenye kurasa 10 iliyoonwa na Gazeti la Nation, Fifa imeamua kumuanzishia kesi Owino kwa kukiuka maadili nyeti ya shirikisho hilo la kimataifa kati ya Juni 2009 na 2011.

 

Kwa mujibu wa ripoti ya Fifa iliyotolewa Septemba 2018, Owino, 37, kupitia meseji 177 kati yake na mpanga matokeo mkubwa wa kimataifa, Wilson Raj Perumal, ilibainika kuwa nyota huyo na jamaa huyo walikubaliana auze mechi za kimataifa zinazoihusisha Kenya.

Fifa imesema Owino, 37, alikubali akiwa pamoja na baadhi ya wachezaji wa Harambee Stars wacheze sawasawa na maelekezo ya Perumal.

 

Taarifa zaidi za mechi 14 zilizotajwa kama uthibitisho, bado zimeshikiliwa na Idara ya Maadili ya Fifa, ambayo iliwasiliana na Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) Agosti 10, 2018 ikihitaji mikataba ya Owino.

 

Perumal aliwahi kufungwa nchini Finland na Hungary kwa makosa ya kupanga matokeo. Owino aliichezea Simba kwa msimu mmoja wa 2007-08. Pia aliwahi kuichezea Yanga mwaka 2009.

Comments are closed.