The House of Favourite Newspapers

Beki Simba: Ubingwa Bado ni Mgumu “Kwa sasa Huwezi Kusema Nani Atakuwa Bingwa”

0

BONIPHACE Pawasa, beki wa zamani wa kikosi cha Simba, amesema kuwa kwa sasa bado vita ya ubingwa ni ngumu kutokana na kila timu kuhitaji kushinda.

 

Ni mbio za mafahali wawili kati ya Yanga ambao ni vinara pamoja na Simba ambao ni mabingwa watetezi, wanapambana kuweza kutwaa taji hilo.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Pawasa alisema kuwa kila timu ina nafasi ya kufanya vizuri kutokana na mechi ambazo wanacheza.

 

“Kwa sasa huwezi kusema nani atakuwa bingwa kwa kuwa kila timu ina mechi mkononi na pointi huwa inahesabiwa baada ya kuchukua kwenye timu husika.

 

“Ninachoweza kusema ni kwamba ushindani umekuwa mkubwa hivyo bado kuna muda unahitajika ili kuweza kujua nani atakuwa bingwa ila yule ambaye atafanya vizuri atakuwa bingwa,” alisema Pawasa.

 

Yanga na pointi 48 ikiwa haijapoteza mchezo baada ya kucheza mechi 18 na Simba ipo nafasi ya pili na pointi 37 imecheza mechi 17.

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

Leave A Reply