The House of Favourite Newspapers

Beki ya Yanga Uchochoro, Wameruhusu Mabao 10

Kikosi cha timu ya Yanga.

REKODI zinaonyesha kwamba beki ya Yanga iliyo chini ya Kelvin Yondani kwenye Ligi Kuu Bara imekuwa uchochoro. Kwenye michezo 15 ya mwanzo wa ligi ambayo Yanga walicheza sawa na michezo ya Simba waliyonayo kwa sasa tayari walikuwa wameruhusu kufungwa mabao 10.

 

Licha ya kushinda michezo yao yote kwa wakati huo kutokana na safu makini ya ushambuliaji bado wamepotezwa na Simba kwa upande wa mabeki. Beki ya Simba ambayo ipo chini ya Muivory Coast, Pascal Wawa, kwenye michezo 15 waliyocheza wameruhusu mabao matano pekee.

 

Hivyo Februari 16 kutakuwa na vita mpya ya kulinda rekodi ama kutibua rekodi kutokana na mazingira ya mchezo ambavyo yatakuwa.

Comments are closed.