The House of Favourite Newspapers

Beki Yanga Mamadou Doumbia Afiwa na Baba Yake Mzazi

0

 

Beki wa Kimataifa wa Yanga, Mamadou Doumbia mwenyeji wa Mali amefiwa na Baba yake jana huko Bamako nchini Mali. Taarifa kutoka kwenye ukurasa wa Intagram wa Yanga imeeleza kuwa ‘Klabu ya Yanga imepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Baba mzazi wa mchezaji wetu Mamadou Doumbia kilichotokea jana nchini Mali. Mama dou Doumbia anatarajia kusafiri Asubuhi ya leo kuelekea Mali kwaajili ya kushiriki taratibu za mazishi’ ‘Kwa niaba ya wanachama, wapenzi na mashabiki wa Yanga Uongozi wa klabu ya Yanga unatoa pole kwa mchezaji wetu Mamadou Doumbia na familia yake yote kwa msiba huu ”

Ikumbukwe kuwa Mamadou Doumbia ni beki kitasa aliyesajiliwa dirisha dogo akitokea timu ya Stade Malien ya kwao Mali lakini tangu ajiunge na vigogo hao wa jangwani hajawahi kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha Yanga pamoja na kwamba awali alikua mchezaji anayetazamiwa kufanya makubwa akiwa na kikosi cha Yanga.

Leave A Reply