Beki Yanga: Nabi Atawanyoosha Simba

BEKI anayeimbwa sana kwa sasa ndani ya Yanga tangu alipoanza kupewa nafasi ya kucheza, Dickson Job, amesema kuwa kuna mambo yameanza tangu kuja kwa kocha Nasreedin Nabi na huenda wakashinda dhidi ya Simba kirahisi.

Job alisema kama kocha huyo akipewa muda na yeye mwenyewe akawa mtulivu, basi kuna mazuri ataifanyia Yanga na hata kwenye mchezo dhidi ya Simba kuna kitu anakitengeneza kitakachowashangaza wengi.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Job alianza kwa kujitaja mwenyewe kuwa yupo fiti na tayari kwa kucheza dhidi ya Simba na akiongeza kwa kumwaga sifa kwa Nabi akisema kwa mbinu anayoitengeneza anaona kabisa wanakwenda kuwafunga Simba licha ya kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kwao.

“Kwanza kwa upande wangu niko poa na tayari kucheza mchezo huo kama kocha ataniamini tena. Kuhusu uwezo wa kocha binafsi sina shaka naye kwani ameonyesha utofauti kidogo kwa muda mfupi aliokaa klabuni.

“Kama watampa muda zaidi na yeye mwenyewe kutulia, naamini anaweza kutengeneza timu bora zaidi,” alisema Job.

ISSA LIPONDA,
Dar es SalaamTecno


Toa comment