BELLA, FIRST CLASS KUKINUKISHA KRISMAS HII

King of The Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’

KAMA ulikuwa ukijiuliza sikukuu hii ya Krismas huende wapi jibu simpo tu. Uwanja wa Kimataifa wa Burudani, Dar Live unatarajia kumshusha siku hiyo King of The Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ pamoja na Kundi la Taarab la First Class chini ya kiongozi wao Prince Amigo.  

Akizungumza na Ijumaa, Mratibu na Meneja wa Dar Live, Rajab Mteta ‘KP Mjomba’ alisema kuwa, katika usiku huo unaotambulika kama Walete Dar Live, Bella anatarajiwa kuondoka na kijiji.

 

“Wote tunajua kuwa, Bella hajawahi kukosea jukwaani, sasa katika sikukuu hii ya Krismas atashuka na bendi yake ya Malaika na kupiga vibao vyao vyote vikali kuanzia Nakuhitaji, Msaliti na nyingine nyingi,” alisema KP na kuongeza;

“Pia tutakuwa na kundi la Taarab la First Class chini ya Amigo likiwa na wakali kibao akiwemo Mosi Suleiman, unaachaje sasa kuja Dar Live kuwashuhudia. Mbali na hao tutakuwa na wakali wa Singeli kama vile Yuda Msaliti na Vailasi Mdudu.”

 

Kiingilio katika sikukuu hiyo kitakuwa ni shilingi 10, 000 wakati burudani kwa watoto itakayoanza saa 2:00 Asubuhi hadi 12:00 Jioni itakuwa ni shilingi 3,000 tu.

Stori: Mwandishi Wetu

Toa comment