The House of Favourite Newspapers

Bella kuja na sapraizI Dodoma, Julai 22

0

BELLAKING of The Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ anatarajiwa kuja na bonge la sapraizi katika shoo ya kihistoria itakayofanyika Julai 22, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Royal Village, Dodoma.

Akizungumza na Risasi Vibes mratibu wa shoo hiyo, Renatus Gregory alisema kuwa usiku huo pia kutakuwa na DVD za miaka 10 ya Bella tangu aingie kwenye muziki.

“Siku zote Bella awapo jukwaani ni mtu wa sapraizi hivyo mashabiki waje kwa wingi washuhudie alichowaandalia, kila atakayeingia ukumbini ataamini ninachomaanisha,” alisema Renatus.

Usiku huo kiingilio kitakuwa shilingi 30,000 kwa VIP na kawaida shilingi 10,000.

Leave A Reply