The House of Favourite Newspapers

Bella, msanii wanaswa na misokoto hotelini

0

IMG_0104Msanii wa filamu Isabela mpanda ‘Bella’  akiwa kwenye pozi la kimahaba na  Sitta Richard Majani ‘Staric’.

Erick Evarist
Baada ya kumfumania aliyekuwa mpenzi wake, Kalama Bakari ‘Luteni Kalama’, Miss Ruvuma 2006, Isabela mpanda ‘Bella’ amenaswa hotelini akiwa na msanii wa Bongo Fleva, Sitta Richard Majani ‘Staric’ wakiwa na misokoto iliyodaiwa kuwa ni ya bangi.

Staric anayetamba na Wimbo wa Kata na Bella walinaswa hivi karibuni katika Hoteli moja iliyopo Mikocheni jijini Dar baada ya mtu wao wa karibu kuwapiga picha za kimahaba kwenye simu ya msanii huyo wa Bongo Fleva kisha kuzihamishia katika simu yake.

IMG_0076

…Wakipozi.

Mtu huyo baada ‘kuwafotoa’ picha hizo ambazo wenyewe walijua ni kwa matumizi yao, aliziiba kijanja na kuwasiliana na Ijumaa.

“Jamani kumbe baada ya Bella kumwagana na Kalama sasa hivi anatembea na msanii wa Bongo Fleva anaitwa Staric na juzi tulikuwa pamoja wakachukua rumu hotelini, wakafanya yao.

“Walivuta sigara kubwa na kunywa pombe sana ni aibu kwa kweli kutokana na kujiachia kihasara. Kabla hawajaanza kufanya mambo, waliniomba niwapige picha sasa mimi nikaziiba bila wao kujua,” alisema mfukunyuku huyo.

IMG_0129

Misokoto waliyonaswa nayo.

Baada ya mtoa ubuyu huyo kumrushia mwanahabari wetu picha za wawili hao, Ijumaa liliwatafuta na kuwasomea mashtaka yao ambapo wa kwanza alikuwa Staric;
Ijumaa: Tumenasa picha zako za kimahaba na Bella, vipi ndiyo shemeji yetu?
Staric: Daah! Mmezipataje? Sikia hayo ni mambo yangu binafsi bwana, si picha tu hizo.
Ijumaa: Vipi kuhusu misokoto iliyoonekana kwenye picha, mlitumia bangi na pombe vya kutosha ee?

IMG_0075Staric: Acheni mambo yenu bwana, sijawahi na wala sitakuja kuvuta hiyo kitu. Hizo zilikuwa ni mfano wa bangi ambazo nitazitumia katika video ya wimbo wangu mpya kuonesha vijana walioathirika na uvutaji wa bangi. Pombe yenyewe sinywi sembuse bangi! Bora hata mwenzangu (Bella) anakunywa lakini havuti bangi.

Kwa upande wake Bella alijibu kwa kifupi na kukata simu: “Jamani mambo mengine si ya kujibu.”

Leave A Reply