The House of Favourite Newspapers

Belle 9 kuja na mkwaju mpya

belle9 (1)Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Abednego Damian ‘Belle 9’

LICHA ya Ngoma yake ya Shauri Zao kutamba katika vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Abednego Damian ‘Belle 9’ yupo mbioni kutoa wimbo mwingine anaotarajia kuuachia hivi karibuni.

Staa huyo ambaye pia alitamba na nyimbo kama Sumu ya Penzi, Nilipe Nisepe, kwa sasa amepiga makazi yake jijini hapa Dar akitokea Morogoro alikokulia.

belle-9-7Akipiga stori na Mikito Jumatano, Belle 9, alisema kuwa kwa sasa anakamilisha kurekodi wimbo wake huo mpya ambao anatarajia kuuachia hivi karibuni.

“Nipo katika mchakato sasa wa kudondoka na ngoma nyingine kabisa baada ya hii ya Shauri Zao ambapo wimbo huo naweza kuuachia hewani hivi karibuni,” alisema Belle 9.

Comments are closed.