The House of Favourite Newspapers

Ben Affleck Ampotezea J-Lo, Aangukia Penzini na Angelina Jolie!

Ukisikia zege halilali ndiyo hii sasa! Miezi michache iliyopita, staa wa filamu Hollywood, Ben Affleck alikamilisha mchakato wa talaka na mwanadada Jennifer Lopez.

Mpaka wanafikia hatua ya kupeana talaka, J -Lo akiwa ndiye aliyeshikia bango suala hilo, Ben Affleck alikuwa anaonekana ni kama anakaribia kudata! Mapenzi yalikuwa yakimuendesha mbio kisawasawa.

Guess what? Hata miezi minne haijaisha, jamaa keshaangukia tena penzini na safari hii, ni kwa mwanadada mwingine staa mkubwa kama ex wake, Angelina Jolie.

Japokuwa Jolie ni ex wa rafiki yake wa karibu, Brad Pitt, unaambiwa jamaa hajali chochote kwa sababu walishamwagana kitambo.

Hata hivyo, bado mambo ni chini kwa chini lakini wadaku wanakwambia ‘soon’ kila kitu kitakuwa wazi.