The House of Favourite Newspapers

Ben Pol aanza mwaka na Ben Pol

0

benpol2Ben Pol.

Khadija Mngwai, Dar es Salaam
MWANAMUZIKI wa muziki wa Kizazi kipya ‘Bongo Fleva, Benard Paul (Ben Pol) amefunguka kwa kusema kuwa anauanza mwaka wa 2016 kwa kutoa albamu yake iliyobeba nyimbo 13, mwanzoni mwa mwezi wa pili.

Akizungumza na Championi Jumatano, Pol amesema kuwa wasanii wengi wamekuwa wakiuchukulia muziki huo ni wa kawaida tu kwa kuhitaji kujiingizia kipato na siyo kuwa ‘serious’ na matokeo yake wanaishia kutoa nyimbo moja au mbili ili kupata shoo.

BEN-POL-1“Nimejipanga kuweka rekodi ya pekee mwaka huu kwa kuachia albamu yenye nyimbo 13 ambayo natarajia kuitoa mwanzoni mwa mwezi wa pili ambayo itakwenda kwa jina la Ben Pol.

“Wanamuziki wengi wamekuwa wakiuchukulia muziki kama biashara na sio ‘serious’ katika kuhakikisha wanafanya vyema na kuweza kuukuza kwa kuwa wabunifu na badala yake kutegemea shoo mara baada ya kutoa nyimbo moja au mbili,” alisema Pol.

Leave A Reply