Ben Pol katika pozi kwenye studio za Global TV Online leo.
Ben Pol akiwa ametulia na Mtangazaji wa Global TV Online, Shorvieny Mohammed.
Mhariri Msaidizi wa Gazeti la Ijumaa Wikienda, Gabriel Ng’osha akipozi na Ben Pol.
Mwandishi wa Hadithi na Mikasa wa GPL, Nyemo Chilongani akiwa na Ben Pol.
Ben Pol na Mhariri wa Habari za Burudani GPL, Andrew Carlos katika pozi.
Ben Pol baada ya kumaliza mahojiano na Global TV Online.
Boniphace Ngumije
MKALI wa Muziki wa RnB kutoka Bongo, Benard Paul ‘Ben Pol’ amefunguka kuwa anachumba maalumu nyumbani kwake kwa ajili ya kusikilizia muziki pekee, ambapo mara kwa mara akiingia ndani ya chumba hicho hufungulia sauti ya juu na kuanza kufurahia nyimbo mbalimbali.
Akichonga ndani ya Mtu kati ya Global TV Online leo, Ben Pol alisema sababu kubwa ya kuamua kutenga chumba kwa ajili ya kazi hiyo ni kupata wasaa mzuri wa kufaidika na usikilizaji wake ikiwa ni pamoja na kujifunza baadhi ya maujanja wanayoyafanya wasanii wenzake walioko kwenye tasnia ya muziki.
“Unajua kwa msanii anayehitaji kuuendeleza zaidi uwezo wake wa kuimba ni lazima ajifunze kila siku, kwa kuliheshimu hilo, nimetenga chumba maalumu kwa jili ya kusikilizia muziki, mara nyingi katika chumba hicho nikiingia nafungulia redio katika sauti ya juu pia napendelea kuingia nikiwa peke yangu,” alisema Ben Pol.
Usikose kutazama Mahojiano yake ndani ya Global TV Online hivi karibuni