The House of Favourite Newspapers

Ben pol ataja sababu ndoa ya kimyakimya!

DAR ES SALAAM: Staa mkubwa wa muziki wa RnB Bongo, Benard Paul ‘Ben Pol’ ametaja siri ya kufunga ndoa ya kimyakimya na mwanadada tajiri wa nchini Kenya, Anerlisa Muigai.  Ben Pol na Anerlisa walidaiwa kufunga ndoa ya kimyakimya miezi kadhaa iliyopita na kufuatiwa na pati ya kimyakimya iliyohudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wa karibu. Harusi ya Ben Pol na Anerlisa ilifanyika huko Runda jijini Nairobi, Kenya. Akizungumza na Gazeti la Ijumaa juu ya mkewe huyo kuhamia jumla nchini Tanzania, Ben Pol alikiri kufunga ndoa hiyo.

Ben Pol alikwenda mbali zaidi na kutoa siri kuwa sababu ya kufanya tukio hilo kuwa la kimyakimya ni kwamba alitaka liwe ni tukio la kwao binafsi. Alisema; “Ni kweli nilifunga ndoa, lakini sikutaka kuitangaza kwa sababu lilikuwa ni jambo la kifamilia zaidi. “Watu wana namna tofauti za kuoneshana mapenzi. “Kwangu mimi muziki ndicho kitu ninachpenda kukizungumzia hadharani, lakini mambo binafsi ningependa yaendelee kuwa ya binafsi.”

Stori: Neema Adrian ,Ijumaa

Comments are closed.