BEN POL ATAMBULISHA WIMBO MPYA WA ‘WAPO’ (PICHA +VIDEO)

Staa wa Bongo Fleva, Bernard Paul ‘Ben Pol’ akisaini kitabu cha wageni alipotembelea ofisi za Global Group, Sinza-Mori jijini Dar es Salaam leo.

STAA wa Bongo Fleva, Bernard Paul ‘Ben Pol’ leo alifika ndani ya ofisi za Global Group maalum kwa kutambulisha ujio wake mpya wa wimbo wa Wapo ambapo ameeleza namna mpenzi wake, Anerlisa,  alivyohusika katika kuandaa video ya wimbo huo.

Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa, Richard Manyota (kushoto) akiongea jambo na Ben Pol.

Akizungumza katika Kipindi cha Bongo 255 kinachoruka kupitia +255 Global Radio, Ben Pol alisema  kabla hajaachia wimbo huo mchumba wake huyo mwenye asili ya Kenya alikuwa halali akihakikisha video hiyo iwe nzuri.

Mtangazaji wa Global TV Online, Judith Mlwale (kushoto) akisalimiana na Ben Pol.

“Ane (Anerlisa) amenisaidia sana katika video hii ya Wapo. Nimekesha naye akihakikisha kila nguo ninayotumia kwenye video ipo sawa. Ana jicho zuri katika ubunifu kuanzia mimi,  hadi modo aliyetumika katika video ile amemtafuta yeye na kumvalisha,” alisema Ben Pol na kuongeza:

Meneja Mkuu wa Global Group, Abdallah Mrisho,  akiongea jambo na Ben Pol.

“Alikuwa yupo karibu kwa kila kitu hadi nyuma ya ile video amehusika wewe fanya hivi, wewe fanya vile yaani ni dairekta wa pili wa video ile,” alisisitiza.

Pia alizungumzia kumtungia wimbo mpenzi huyo akisema upo tayari jikoni.

“Kuna wimbo nimeshamwandikia lakini nafikiri katika nyakati za harusi huko ndiko unaweza kutoka,” alisema .

 

Ben Paul akisoma meseji kabla ya kufanya mahojiano na Global Radio.

 

Ben Pol – Wapo (Official Music Video)

Loading...

Toa comment