The House of Favourite Newspapers

BEN POL: KUTOKA GIGY MONEY HADI MONALISA!

Image result for ben pol

Benard Michael Paul ‘Ben pol’MWAKA 2013, taasisi ya vijana inayotambulika kama Youth For Africa (YOA) ilitoa tuzo zake kwa mara ya kwanza zilizotambulika kama Under 30 Youth Awards ambapo usiku huo, staa wa muziki wa R&B Bongo, Ben Pol aliibuka kidedea kupitia kipengele cha Best Male Vocalist Of The Year.

YOA hawakukosea kumpatia tuzo hiyo Ben Pol kwani miaka miwili kabla ya hapo alikuwa ametoka kuchukua tuzo mbili kupitia Tuzo za Muziki za KTMA.

 

Ben Pol ambaye cheti chake cha kuzaliwa kimeandikwa Benard Michael Paul Mnyang’anga ni miongoni mwa mastaa wakubwa katika muziki wa R&B Bongo ambaye ameweza naye kukaa kwa zaidi ya miaka nane bila kushuka kiwango. Tangu alipotoka na ngoma yake ya Nikiku-pata, My Number One Fun, Sam-boira, Maboma, Sophia, Maneno hadi Moyo Mashine ameonesha ni mkali kiasi gani.

 

Kwa sasa Ben Pol ameachia ‘dongo’ jingine linalokwenda kwa jina la Ntala Nawe ambapo ndani ya kichupa amemuuzisha nyago mwigizaji mkongwe wa filamu Bongo, Yvone- Chery Ngatikwa ‘Monalisa’. Katika mahojiano niliyofanya naye, Ben Pol amezungumzia mengi kuhusiana na maisha yake ya kimuziki, huyu hapa;

 

Showbiz: Idea ya Ntala Nawe ilikuwaje?

Ben Pol: Ni wimbo ambao umeandikwa na mtunzi kutoka Kenya anaitwa Ben Soul na alinifikia kutoka kwa Prodyuza Cedo kwa hiyo walinipa hiyo Ntala Nawe nikaifanya.

Showbiz: Kwa upande wa video, mwigizaji Monalisa ametumika kama video queen kwa mara ya kwanza na mara ya mwisho ulimtumia mwenye ‘profeshino yake’ Gift Stanford ‘Gigy Money’ katika video yako ya Tatu, uliwezaje kumshawishi?

 

Ben Pol: Nilitaka kufanya video na mtu anayeheshimika kwenye jamii na mwenye mashabiki kutokana na ukubwa wa wimbo wangu ndiyo nikaangukia kwa Monalisa.

Aliniambia hajawahi kufanya video ya muziki wowote, lakini kwa heshima yangu na kwa kuwa anapenda kazi zangu akanikubalia ndiyo tukafanya.

Showbiz: Tumekuwa tukishuhudia ukifanya kolabo nyingi na Maua Sama kwa upande wa wasanii wa kike, lakini wewe kama wewe hujawahi kumshi-rikisha zaidi ya kushir-ikishwa?

Ben Pol: Kuna wimbo ambao nimems-hirikisha Maua, lakini bado haujatoka. Nimefanya naye ngoma nyingi sana kwa hiyo mashabiki wakae mkao wa kusikia tu.

 

Sho-wbiz: Kuna wasanii kutoka nje kama Emm-anuel Austin (Ujerumani) na Kiss Daniel (Nigeria) ambao umeshashiriki nao kufanya kolabo za kimataifa, mashabiki watarajie wasanii gani wengine?

Ben Pol: Kwa sasa nataka kufanya kazi na wasanii wapya kwa hiyo mashabiki wategemee kuniona ninafanya nao kazi na pia kutanua soko langu la kimataifa kwa kufanya shoo kwenye majukwaa makubwa ya nje ya nchi.

 

Showbiz: Ben Pol kama Ben Pol una idea ya kuja na albamu?

Ben Pol: Mwaka jana Desemba nilitoa albamu yangu ya kwanza ilikuwa inaitwa Best of Ben Pol, lakini natarajia kutoa albamu mara nyingi zaidi kwani naiona fursa ya kutoa albamu kwenye mitandao.

Showbiz: Kuuza albamu mitandaoni inalipa kweli?

Ben Pol: Ujue kuna mashabiki wengi nje ya nchi wanatamani sana kusikia muziki wa Tanzania kwa hiyo ukiweka albamu kwenye mitandao hiyo mikubwa kama vile iTunes na Amazoni japokuwa ni kidogokidogo, lakini inaongezeka kwa kasi sana.

 

Showbiz: Mara ya mwisho ulifanya kolabo na Jux ikabamba sana, je, mna mpango wa kufanya projekti maalum kama Rostam (Roma na Stamina)?

Ben Pol: Kutengeneza kama kundi kidogo tunaweza kuchelewa, lakini kama mashabiki wanahitaji tunaweza kufikiria. Jux ni mtu ninayeongea naye sana na mashabiki watatusikia sana kwani hata mwaka jana tulifanya ziara ya pamoja na ikabamba sana.

 

Ben Pol: Tukirudi kwenye idea ya Ntala Nawe, tumeona umemtumia Monalisa, je, na yeye akitumia nafasi kukutumia kwenye filamu zake upo tayari?

Showbiz: Ofcourse mimi najua kuigiza, nimeshawahi kuigiza kwenye muvi inaitwa Sunshine, kusema ukweli nina kipaji cha kuigiza sema kwa sababu muziki umenisaidia sana inabidi niwe huko kwa hiyo Monalisa akihitaji kunitumia huko naweza kufanya.

Ben Pol: Tume-ona mastaa wengi wakion-gozana na maba-unsa mfano, Harm-onize, Barnaba, Diamond na wengineo, vipi wewe?

Showbiz: Kuwa na baunsa kusema ukweli sijafikiria kwani naona kama ni mbwembwe labda kama naenda mazingira ya shoo, lakini siyo kwenye kila kitu sijui party ndogo, shopping na nyingine.

Ben Pol: Shoo gani ya kimataifa ambayo unaikumbuka maishani mwako?

 

Showbiz: Shoo tatu ninazozikumbuka, moja nilifanya Kenya nikiwa na Peter wa P Square pamoja na Chioma, ilikuwa kubwa sana, nyingine nilifanya Ujerumani, Munich ilikuwa 2016 ilikuwa shoo ya Kizungu kwani walihudhuria karibu Wazungu tupu.

Showbiz: Una lebo yoyote?

Ben Pol: Sina lebo wala similiki wasanii ila ninawasaidia tu.

Comments are closed.