The House of Favourite Newspapers

Ben Pol: Nimeanza na Kiss Daniel

Bernard Paul ‘Ben Pol’

MWANAMUZIKI Bernard Paul ‘Ben Pol’, hivi karibuni amefunguka kwamba ujio wake mpya na mwanamuziki kutoka Nigeria, Kiss Daniel unaojulikana kwa jina la Zai, ambao yupo mbioni kuuachia ni mwanzo wa kolabo zake za kimataifa kwa mwaka huu.

 

Akichonga na Showbiz Xtra, Ben Pol alisema kwamba mwaka huu amejipanga kwa makubwa na kolabo yake hiyo ni mwanzo wa hayo makubwa ambayo anatarajia kuyatoa kwani anazaidi ya kolabo tatu za kimataifa mwaka huu ambazo zitampeleka ‘level’ nyingine.

Kiss Daniel

“Mwaka huu ninatarajia kutoka na kazi zaidi ya tatu za kimataifa na ujio wangu na Kiss Daniel ni mwanzo wa kazi hizo, mashabiki wangu wakae mkao wa kula,” alisema Ben Pol.

BONIPHACE NGUMIJE

Comments are closed.