BENKI YA ACB YASHEREKEA SIKU YA WANAWAKE, YAWATUNUKIA ZAWADI

Wafanyakazi wa ACB wakiwa kwenye pozi la pamoja katika kurehekea Siku ya Wanawake Duniani.

BENKI ya ACB katika kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani leo imewatunukia zawadi mbalimbali wateja wake wanawake ambao wanafanya vizuri katika benki hususani kukopa mikopo na kurejesha vizuri.

Akizungumza kwenye hafla iliyofanyika kwenye benki hiyo tawi la Ubungo Plaza jijini Dar, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Dora Saria,  amesema wameamua kumtunukia zawadi mwanamama mjasiriamali, Christina Ossunga, ambaye alianza kukopa kwenye benki hiyo kiasi cha shilingi elfu 50,000. ambapo sasa amefikia kiwango cha kukopa shilingi milioni 100. Pamoja na mwanamama huyo, pia benki hiyo imewatunukia zawadi mbalimbali wanawake wengine ambao ni wateja wake.

Naye Christina baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo alisema anaishukuru benki hiyo kwa kumvumilia maana katika harakati za ujasiriamali wake kuna kipindi alikuwa akikumbana na changamoto ikiwemo kuugua na kushindwa kurejesha majeresho lakini alipotoa taarifa kabla haikuwa tatizo kwao.

Matukio katika Picha:

Christina Ossunga akielezea jinsi alivyoweza kumudu kukopa na kurejesha mikopo kwenye benki hiyo ambapo alianza kukopa shilingi 50,000 na kufikia shilingi milioni 100 sasa.

…Akipokea zawadi ya kitenge kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa ACB.

…Akiwa na wafanyakazi wa ACB.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Dora Saria,  akiwa na furaha wakati wa hafla hiyo ikiendelea.

 

HABARI/ PICHA: RICHARD BUKOS/GPL   

Toa comment