The House of Favourite Newspapers

Benki Ya Azania, Selcom Washirikiana Kuboresha Huduma Za Malipo Ya Kidijitali

0
Mkuu wa huduma za Benki Kidijitali wa Benki hiyo Bw. Vinesh Davda akionesha mashine ya kufanyia miamala ya Benki ya Azania. Kushoto ni Meneja Taifa- Biashara wa Kampuni ya Selcom Bw. Geofrey Mwakamyanda. 

Dar es Salaam, 18 Mei 2023:Benki ya Azania, inayomilikiwa na mifuko ya hifadhi za jamii nchini leo hii wamezindua rasmi ushirikiano na kampuni kinara katika huduma za kifedha na malipo kidijitali ya Selcom, ushirikiano wenye lengo la kuboresha huduma za Fedha kidijitali ikiwa ni muendelezo wa kuboresha huduma za Benki hiyo inayokua kwa kasi.

Kwa miaka ya hivi karibuni Benki ya Azania imekuwa ikichukua hatua kubwa kuhakikisha inakua na kuboresha huduma kwa wateja wake.

Meneja Taifa- Biashara wa Kampuni ya Selcom Bw. Geofrey Mwakamyanda kushoto akielezea jinsi ushirikino huo utakavyoboresha huduma kwa wateja.

Kupitia ushirikiano huu, mteja wa Benki ya Azania ataweza kupata huduma za kifedha kupitia mawakala wa Selcom, ikiwemo kuweka na kutoa fedha kwa kadi au bila ya kadi, kujua salio, na kwa Mawakala wa Benki ya Azania wataweza kuongeza salio huku tozo zikiwa ni zilezile bila ongezeko na faida nyinginezo nyingi.

Pia huduma ya malipo kwa kadi (Merchant’s payment) inayotolewa na Benki ya Azania sehemu mbalimbali kama vile maduka makubwa, hoteli na sehemu za starehe, hospitali, vituo vya kuuza mafuta nk. Sasa kupitia Selcom huduma hiyo imeboreshwa na kuwa na wigo mpana zaidi na sasa mteja wa Azania ataweza kutumia kadi ya Visa, UnionPay, Mastercard, au American Express kufanya malipo hayo.

Hivi ndivyo ushirikiano huo ulivyozinduliwa.

Akiongea katika uzinduzi huo, Mkuu wa huduma za Benki Kidijitali wa Benki hiyo Bw. Vinesh Davda alisema kuwa ‘’huu ni muendelezo Katika kuendelea kuwajali wateja wetu na watanzania kwa ujumla kwa kutuunga mkono tumehakikikisha kila mara tunaboresha huduma zetu na kuendana na kasi ya maendeleo na ukuaji wa Teknolojia uliopo’’.

“Huduma yetu imeboreshwa zaidi na sasa inauwezo wa kutumia kadi za aina nyingi zaidi ikiwemo Visa, Mastercard, UnionPay na American Express, hivyo kuwaondolea usumbufu wateja wetu kwa kiasi kikubwa, lakini pia kuongeza mchango katika ushirikishwaji wa kifedha na kupunguza matumizi ya pesa taslimu’’.

Meneja huyo alimalizia kwa kusema kuwa huduma hii itawapa urahisi zaidi wateja wa Benki ya Azania waliopo maeneo ambayo hakuna tawi la Benki hiyo kwa kutembelea Wakala yeyote wa Selcom ambao wanapatikana takriban nchi nzima na hapo watapata huduma zote ambazo wangezipata kupitia mawakala wa Azania.

Akiongelea ushiriki wa Selcom katika maboresho na mapinduzi ya huduma za kifedha na malipo nchini, Meneja Taifa- Biashara wa Kampuni ya Selcom Bw. Geofrey Mwakamyanda anabainisha kuwa anajisikia faraja kwa kuendelea kuaminika kwa kampuni ya Selcom kwa wadau wa sekta ya fedha wakiwemo Azania Bank.

“Kwa takribani miaka 20 sasa Selcom imekuwa kinara kwenye utoaji wa huduma za kifedha na malipo, “Agency Banking” huduma za kibenki kupitia kwa mawakala wa Selcom Huduma waliosambaa nchi nzima ni miongoni mwao.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Azania na wageni waalikwa wakishuhudia tukio hilo.

Hii inasaidia kuongeza ushirikishwaji wa kifedha “financial inclusion” kwa watanzania wote bila kubagua kipato chao au mahali walipo. Hivi sasa hauna haja ya kutafuta wapi palipo na tawi au ATM ya Azania Bank ili kupata huduma, mawakala wa Selcom Huduma waliopo hapohapo mtaani kwako wapo tayari kukuhudumia.”

Akiongezea kuhusu Huduma nyingine ya malipo kidijitali, Mwakamyanda anaweka bayana. “Dunia ilipo sasa katika nyanja ya malipo hauhitaji kuwa na pesa taslimu. Kuna sababu za kiusalama, urahisi wa kulipa kwa simu au kadi na nyingine nyingi zinazopelekea njia za malipo kama Selcom Pay kuchukuliwa kwa ukubwa unaostahili. Ewe Mtanzania usiachwe nyuma”. Alimaliza kusema.

Leave A Reply