The House of Favourite Newspapers

Benki ya CRDB Yatunukiwa Tuzo za ‘Benki Bora’ na ‘Benki Salama’ Tanzania na Jarida la Global Finance

0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto), akipokea tuzo ya ‘Benki Bora Tanzania’ kutoka kwa Joseph Giarraputo, Mwanzilishi na Mhariri Mkuu wa Global Finance, katika hafla iliyofanyika Washington D.C. tarehe 26 Oktoba 2024. Katika hafla hii, iliyofanyika sambamba na Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, Benki ya CRDB pia ilitunukiwa tuzo ya ‘Benki Salama.

Benki ya CRDB imetambuliwa kwa mara nyingine kama kinara katika sekta ya benki Tanzania kwa kushinda Tuzo ya ‘Benki Bora Tanzania’ na ‘Benki Salama Tanzania’ zilizotolewa na Jarida la Global Finance kwenye hafla ya 31 ya Mwaka ya Tuzo za Benki Bora.

Tuzo hizo zimetolewa katika hafla iliyofanyika sambamba na Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia huko Washington, D.C. Hii ni mara ya tano mfululizo kwa Benki ya CRDB kushinda tuzo ya Benki Bora Tanzania na mara ya pili mfululizo kwa Benki Salama Tanzania – ikidhihirisha uimara wa Benki hii katika sekta ya fedha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema tuzo hizi ni kielelezo cha utendaji bora wa Benki hiyo na ishara ya kuwa ipo kwenye njia sahihi ya ukuaji – kutoa huduma za kipekee kwa wateja wake, thamani kwa wanahisa, na kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta ya fedha nchini.

Nsekela amewashukuru wateja na wadau wa benki hiyo, pamoja na wafanyakazi kwa kuendelea kuifanya Benki ya CRDB, kuwa ‘Benki Bora na Kiongozi’ nchini.

Leave A Reply