The House of Favourite Newspapers

Benki ya Exim, Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kuendesha Kampeni Mikoa Mitano

 

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano kutoka Benki ya Exim, Stanley Kafu akichangia damu kwenye kampeni ya kuchangia damu iliyoandaliwa na Benki ya Exim kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) iliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Exim Bank imekuwa mdau mkubwa wa uchangiaji damu kwa miaka kadhaa sasa na hii ni sehemu ya mpango wa kitaifa wa uchangiaji damu unaoratibiwa na Benki ya Exim kwa kushirikiana na NBTS utakaofanyika katika mikoa mitano. Kushoto ni Mtaalamu wa Maabara, Gisbert Ruseruka.

 

Benki ya Exim kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) imeandaa mpango wa kitaifa wa uchangiaji damu ambapo watazunguka kwenye mikoa mitano kuhamasisha wananchi kuchangia damu kwa hiyari.