The House of Favourite Newspapers

Benki ya NBC, Wafanyakazi Wakabidhi Msaada Kwa Wahanga wa Mafuriko Hanang

0
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa benki ya NBC Bw Godwin Semunyu (wa tano kulia) akiwaongoza wafanyakazi wengine wa benki hiyo kukabidhi kwa  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dk. Jimmy Yonaz (wa tatu kushoto) msaada wa fedha taslimu kiasi cha sh milioni 10, chakula, nguo na mablanketi kwa ajili ya wahanga wa mafuriko Wilayani Hanang, mkoani Manyara. Msaada huo wenye jumla ya thamani ya sh milioni 20 umekabidhiwa leo wilayani humo.

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) sambamba na wafanyakazi wa benki hiyo leo wamekabidhi msaada wa fedha taslimu kiasi cha sh milioni 10, chakula, nguo na mablanketi kwa wahanga wa mafuriko Wilayani Hanang, mkoani Manyara.

Msaada huo wenye jumla ya thamani ya sh milioni 20, pamoja na fedha taslimu unahusisha mchele, maharage, unga na mafuta ya kupikia vyote vikiwa na  jumla ya tani 3.5.

Msaada huo umekabidhiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa benki ya NBCM  Bw Godwin Semunyu kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw Theobald Sabi.

Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Singida Bi Asia Chambega (wa pili kulia) akikabidhi kwa  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dk. Jimmy Yonaz (wa tatu kushoto) msaada wa chakula, nguo na mablanketi kwa ajili ya wahanga wa mafuriko Wilayani Hanang, mkoani Manyara. Msaada huo wenye jumla ya thamani ya sh milioni 20 umekabidhiwa leo wilayani humo.

 

Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, Bw Semunyu aliekuwa ameambatana na baadhi ya maofisa wa benki hiyo waliowakilisha wafanyakazi wengine wa benki hiyo, alisema NBC inatoa salamu za pole kwa wahanga wa tukio hilo, serikali na Watanzania kwa ujumla na kwamba imepokea kwa huzuni kubwa taarifa za athari zilizotokana tukio hilo ikiwemo vifo na upotevu wa mali.

Alisema benki hiyo inaungana na watanzania kwa ujumla katika kuwafariji wahanga wa tukio hilo kwa hali na mali na zaidi kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu wote  waliojeruhiwa na waliopoteza maisha katika janga hilo.

Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Babati Bw Rodgers Masolwa (wan ne kulia) sambamba na Meneja Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Benki hiyo Bi Brendansia Kileo (wa tatu kulia) wakikabidhi kwa  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dk. Jimmy Yonaz (wa tatu kushoto) msaada wa chakula, nguo na mablanketi kwa ajili ya wahanga wa mafuriko Wilayani Hanang, mkoani Manyara. Msaada huo wenye jumla ya thamani ya sh milioni 20 umekabidhiwa leo wilayani humo.

“Tumeamua kutumia kiasi tulichanacho kama taasisi na pia kama wafanyakazi mmoja mmoja kuwasaidia ndugu zetu wanaopitia wakati mgumu kwasasa kutokana na janga hili baya. Pamoja na fedha kiasi pia tumewaletea vyakula mbalimbali ikiwemo unga, mchele, maharage na mahitaji muhimu kama vile mablanketi na shuka ili viwasaidie kwa kipindi hiki cha mpito. ”

“Pia tunashukuru sana serikali yetu na jamii kwa ujumla kwa kusimama imara na kuonyesha ushirikiano mkubwa katika kusaidia wahanga na majeruhi wa janga hili. Tumefarijika kuona wahanga wanaendekea kupata faraja kupitia misaada mbalimbali inayoendelea kutolewa na wadau mbalimbali pamoja na serikali. Nasi tunaahidi kuendelea kusaidia zaidi kadili iwekezanavyo,” alisema Semunyu.

Baadhi ya maofisa wa benki ya NBC wakishusha shehena ya chakula, nguo na mablanketi kwa ajili ya wahanga wa mafuriko Wilayani Hanang, mkoani Manyara. Msaada huo wenye jumla ya thamani ya sh milioni 20 umekabidhiwa leo wilayani humo.

Akipokea msaada huo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dk. Jimmy Yonaz aliishukuru benki ya NBC na wafanyakazi wa benki hiyo kwa kuona umuhimu wa kuwafikia wahanga wa mafuriko hayo   hatua inayothibitisha nia ya dhati ya benki hiyo katika kushirikiana na jamii.

 

Leave A Reply