The House of Favourite Newspapers

Benki Ya NBC Yatoa Gawio La Shilingi Bilioni 6 Kwa Serikali

0
Msajili wa hazina, Nehemia Mchechu.

Dar es Salaam Mei 17, 2023:  Benki ya NBC leo imetoa gawio la shilingi bilioni 6 kwa Serikali, ikiwa ni sehemu ya faida iliyopatikana katika kipindi cha mwaka 2022. Serikali ni mmoja ya wanahisa wa benki ya NBC, ikimiliki aslimia 30 ya hisa.

Akiongea wakati wa makabidhiano ya hundi, msajili wa hazina Nehemia Mchechu aliipongeza benki ya NBC kwa utendaji mzuri uliowezesha kupatikana kwa faida nzuri.

Mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo, Elirehema Doriye.

“Serikali inaridhishwa na utendaji wa benki ya NBC. Ikiwa kama mwanahisa, Serikali inafurahi kuona uwekezaji wake unakuwa wenye tija. Kiasi cha shilingi bilioni 6 tulizopokea leo, zitasaidia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo,” alisema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo Elirehema Doriye alisema, mafanikio ambayo benki imepata yamechangiwa na uaminifu ambao wateja wamejenga kwa benki.

Baadhi ya wageni waalikwa wakishuhudia tukio hilo.

“Tunayofuraha kuendelea vyema katika kuyafikia malengo yetu ikiwa ni pamoja na kujitanua na kuwekeza zaidi katika teknalojia huku tukitoa uzoefu mpya wa huduma za kibenki kwa wateja wetu.

Faida yetu kabla ya kodi imekua kwa 36% kufikia shilingi bilioni 81.9 kutoka shilingi bilioni 60 mwezi Disemba 2021. Faida hii imetuwezesha kutoa gawio la shilingi bilioni 20 kwa wanahisa wetu ikiwamo Serikali ambayo leo tunakabidhi hundi ya shilingi bilioni 6,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Theobald Sabi akizungumza na vyombo vya habari baada ya kutoa gawio hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Theobald Sabi aliishukuru Serikali kwa kutengeneza mazingira rafiki ya biashara ambayo yameiwezesha benki yake kukua siku baada ya siku.

Utendaji na faida tuliyopata ni uthibitisho wa mazingira mazuri ya biashara ambayo Serikali Imeyatengeneza ambayo yametuwezesha kuwafikia wateja wengi zaidi na kutengeneza faida zaidi. Tutaendelea kufanya uwekezaji kwenye upanuzi wa mtandao wetu wa kibenki na kuwekeza zaidi katika teknalojia ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu.

Leave A Reply