The House of Favourite Newspapers

Benki ya NCBA Kutumia Ubunifu wa Kidigitali Kuboresha Huduma Kwa Wateja

0
Wafanyakazi wa Benki ya NCBA wakiwa katika picha ya Pamoja, katika halfa ya sherehe ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, asubuhi ya leo.

 

 

Dar es Salaam, tarehe 3 Oktoba. Benkiya NCBA Tanzania Limited (NCBA) imeendelea kusisitiza juu ya uwekezaji wake katika ubunifu wa kidigiti ili kuboresha huduma kwa wateja wake, jambo ambalo benki inaamini litachochea kusambaa kwa huduma za kifedhanchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NCBA Julius Konyani akiongea katika hafla ya hafla ya wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo.

 

 

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benkiya NCBA, Julius Konyani, wakati wa hafla ya wiki ya huduma kwa wateja iliyohudhuriwa na wafanyakazi na wateja wa NCBA katika jengo la makao makuu lililopo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NCBA Julius Konyani, akiwa katika picha ya pamoja na wateja wa benki hiyo, kutoka kushoto Mbaraka Kihame, Amina Aly, Dennis Chacha na Serphin Lusala.

 

Konyani alisema, “Kupitia mbinu yetu ya kwanza ya kidijitali, tutaendelea kubuni na kutumia nyenzo bora za kiteknolojia katika huduma kwa wateja, ili kuendelea kutoa huduma za kipekee za kifedha na bidhaa zinazozidi matarajio ya wateja, na viwango vinavyokubalika kimataifa,”

 

Aliendelea kwa kusema” Ukubwa na kiwango katika biashara ni muhimu na vinatupa NCBA nafasi ya kuwapa wateja uchaguzi mpana wa bidhaa na mbinu za utoaji huduma hizo.  Teknolojia yetu imara inatengeneza mawasiliano imara kuhusu huduma safi kwa wateja watumiapo bidhaa na huduma zetu katika matawi mbalimbali”.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, aliwataka watumishiwa NCBA kuendelea kufanyakazi kwa bidii ili kuwafurahisha wateja kwa kuwapa huduma za daraja la kwanza pamoja na kuhudumia wateja kwa ufanisi usio wa kawaida, uthabiti, na usikivu.

 

Amina Ally mmoja wa wateja wa NCBA alionyesha dhamira yake kali na furaha kuelekea huduma za kibenki za NCBA. Alisema “Huduma zao nazifurahia, watu wao ni wasikivu. Nikiwa na tatizo lolote kama nahitaji mkopo napata ushauri, wananipa mwongozo mzuri katika jambo lolote lile ninalotakakufanya”.

 

Kwa upande mwingine, Seraphin Lusala mteja mwingine wa NCBA, alibainishakuwa “Huduma za kadi ya mkopo ya NCBA ni nzuri kwangu. Ninathamini sana huduma zao za msaada kwa wateja,” Nukuu hizo zinathibisha nia ya kweli ya NCBA kwa wateja wake na kufuatia hatua ya hivi karibuni ya benki hiyo kuzawadia katika tuzo za Global Banking & Finance kutoka Global Finance Review.

 

Mwaka huu, benki hiyo iliadhimisha wiki yake ya huduma kwa wateja kwa kuwatembelea wateja wao na kusikiliza maoni kutoka kwao ili kujifunza changamoto zao za kuboresha huduma za benki na msukumo wa ukuaji kwa wateja.

Leave A Reply