NMB YAAHIDI KUENDELEA KUCHANGIA JAMII KATIKA SEKTA YA ELIMU NA AFYA 

Mgeni rasmi, Ofisa Habari na Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria kupokea msaada wa Madawati 50 yenye thamani ya Sh. milioni 5 kutoka kwa Meneja wa Tawi la Gongolamboto, Rehema Mwibura (kushoto) na Meneja Mahusiano Biashara za Serikali wa NMB, Faraja Kaziulaya (kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano ya madawati hayo kwa ajili ya Shule ya Msingi Yangeyange iliyopo Msongola Manispaa ya Ilala, jana.

Hafla ikiendelea katika makabidhiano hayo.

Baadhi ya wanafunzi na mgeni rasmi wakifurahia .

 

 

 

SERIKALI Imeishukuru Benki ya NMB kuendelea kusaidia katika Sekta ya Elimu kwa kuchangia madawati baadhi ya Shule zilizo na upungufu na uhitaji mkubwa wa madawati ili wanafunzi waweze kufanya vizuri katika masomo yao.

 

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kupokea madawati 50 yenye thamani ya Sh, milioni 5 kutoka Benki ya NMB, mgeni rasmi Ofisa Habari na Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, aliyemwakilisha Mkurugnezi, aliipongeza benki hiyo kwa kuendelea kuchangia madawati kwa shule zilizo na upungufu.

 

Aidha alisema kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Benki hiyo ikiwa ni jitihada za kuunga mkono juhudi za serikali inayotilia mkazo suala zima la masomo ili kila mtoto aweze kupata elimu.

”Pamoja na Serikali kutangaza kuwa elimu ni bure ili watoto wetu wote waweze kwenda shule, lakini bado inahitahi kushirikiana na wadau wa Elimu kama Benki hii ya NMB ili iweze kufikia lengo la kila mtoto kwenda shule,

Mwaka jana 2018 watoto wa darasa la kwanza walioandikishwa walikuwa ni 22, 000 lakini kwa mwaka huu wameongezeka na kufikia 38,000 hii inaonyesha kuwa hata wazazi wameamka  kuelewa lengo la Serikali kutoa elimu bure, na idadi hii naamini itazidi kuongezeka kila mwaka kutokana na mwamko wa wazazi”. Alisema Tabu.

 

Naye Meneja wa NMB Tawi la Gongolamboto, Rehema Mwibura, alisema kuwa katika kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Sekta ya Elimu na Afya, NMB itaendelea kuwa karibu na Jamii kwa kutoa sehemu ya faida yao kusaidia Sekta hizo zenye uhitaji.

 

”Pamoja na kwamba tumeshatoa misaada ya aina hiyo kwa shule mbalimbali nchini na vituo vya afya lakini bado tutaendelea kurudisha faida tunayoipata kwa jamii kwa kuchangia katika masuala ya kijamii. NMB imekuwa ikichangia sekta za Elimu na Afya kwa kutoa vifaa mbalimbali kama vitanda vya Hospitali na vifaa tiba na Madawati pamoja na viti vyake kwa shule za Msingi na Sekondari.

Loading...

Toa comment