The House of Favourite Newspapers

Benki ya Nmb Yaibuka Kinara wa Tuzo Za TRA

0
Afisa Mtendaji Mkuu  wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna akipokea moja ya tuzo kutoka kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia, Mhe. Nape Nnauye wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni Afisa Mkuu wa Fedha NMB, Bw. Juma Kimori (wa tatu kulia) , Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii  NMB, Bi. Lilian Kisamba pamoja na Meneja wa Kodi NMB, Bi. Janeth Buretta.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia, Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akimpa mkono wa pongezi Afisa Mtendaji Mkuu  wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna.
Viongozi mbalimbali wakipongezana.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia, Mhe. Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na viongozi hao

 

Benki ya NMB imeibuka kinara katika tuzo za mlipa kodi mkubwa zinazotolewa na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA).

Benki hiyo imeshinda tuzo tatu zinazoitambua kama mlipa Kodi Mkubwa nchini kwa mwaka 2021/2022.

Tuzo hizo ni ifuatavyo

 

1 Mshindi wa Kwanza; Taasisi inayozingatia misingi na kanuni bora za ulipaji kodi.

2 Mshindi wa Kwanza; Mlipa kodi mkubwa zaidi katika kundi la taasisi za fedha nchini.

3 Mshindi wa Tatu; Taasisi inayolipa kodi kubwa zaidi nchini (sekta zote).

 

Mafanikio haya ni matokeo ya benki hiyo kuzingatia kanuni bora za ulipaji kodi, ufanisi katika kujiendesha na ubunifu wa suluhishi bora za kifedha zenye manufaa kwa wateja.

Benki ya NMB imedhamiria kuendelea kuendesha biashara yake kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchi ili kuchangia kikamilifu ujenzi wa uchumi wa Taifa.

Leave A Reply