The House of Favourite Newspapers

BENKI YA NMB YAWATAJA 6 WANAOKWENDA KULA BATA DUBAI

Hali ilivyokuwa katika hafla hiyo ya kuwatangaza washindi wa Shindano la MastaBata lililoendeshwa kuhamasisha matumizi ya mfumo wa ‘NMB Mastercard’ au ‘NMB Masterpass’ kwa wateja wao.
Meneja Mwandamizi Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Jilala akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kupatikana kwa washindi watatu wa NMB. 
Meneja Mwandamizi Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Jilala (katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kupatikana kwa washindi watatu wa NMB kwenye shindano la MastaBata ambao pamoja na wenza wao watasafiri kwenda Dubai kwa siku nne kula ‘Bata’. Kulia ni Meneja Huduma za Kadi NMB, Bw. Philbert Casmir pamoja na Meneja Mwandamizi kitengo cha kadi NMB, Bw. Manfredy Kayala (kushoto) wakifuatilia tukio hilo.
BENKI ya NMB imewatangaza wateja watatu ambao wameibuka washindi katika droo ya mwisho ya kampeni ya matumizi ya ‘NMB Mastercard’ au ‘NMB Masterpass’ maarufu kwa jina la ‘MastaBata’.
Wateja hao watatu katika shindano hilo, Einstein Stephen Magebo, Simon Chacha, pamoja na Nuis Paul  Kasambala wakiwa na wenza wao wanatarajia kusafirishwa na Benki ya NMB kwenda nchini Dubai kula Bata kwa siku nne mfululizo safari iliyogharamiwa na NMB kila kitu.
Akizungumza katika tukio hilo, Meneja Mwandamizi Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Jilala alisema washindi hao wamepatikana baada ya kuchezeshwa kwa droo ya mwisho ya Shindano la MastaBata lililoendeshwa kuhamasisha matumizi ya mfumo wa ‘NMB Mastercard’ au ‘NMB Masterpass’ kwa wateja wao.
Aliongeza kuwa mbali na washindi hao wateja kibao wa NMB waliotumia mfumo huo wa malipo pia wamejishindia shilingi 100,000/- kila mmoja na wengine wengi kujishindia simu janja za kisasa aina ya ‘Samsung S9+’.

Comments are closed.