The House of Favourite Newspapers

Benki ya NMB Yazindua Promosheni ya Pata Patia

0

nmb (1)

• Zaidi ya shilling milioni 300 kushindaniwa
Benki ya NMB imezindua mchezo wa bahati nasibu kwa wateja wake ambapo watakuwa na nafasi ya kujishindia kuanzia shilingi 100,000/- hadi shilingi milioni tatu 3,000,000/-. Bahati nasibu hiyo imepewa jina la “Pata Patia” ambapo jumla ya shilingi milioni 300 zitashindaniwa.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkuu wa Kitego cha Wateja Binafsi Boma Raballa alisema kwamba Promosheni ya Weka Ushinde na NMB’ itakuwa na washindi kila wiki na kila mwezi na ni ya kipekee ya wateja wa zamani na wapya

nmb (3)

Bw. Raballa aliongeza kuwa ” Wateja watatakiwa kuweka fedha katika akaunti yoyote ya NMB kiasi cha chini kikiwa ni Shilingi elfu hamsini (50, 000) ili kupata nafasi ya kushinda na zaidi uwekavyo fedha utapata nafasi zaidi ya kushinda. Wateja wanaweza kuweka fedha kupitia tawi letu lolote, NMB Wakala na NMB mobile.”

Promosheni hii itakuwa na droo za kila mwezi ambapo tawi husika la benki ya NMB litawasiliana na washindi 24 kila mwezi kuzungusha gurudumu la bahati katika matawi yaliyochaguliwa na NMB.

NMB imetenga jumla ya shilingi milioni 300 kushindaniwa. Washindi 144 ambao ni wateja wa zamani na wapya wanaweza kushinda hadi shilingi 3,000,000/= kila mmoja; jumla ya washindi 24 watabainishwa kila mwezi kwa kipindi cha miezi sita.

Leave A Reply