BENKI YA TIB YAPATA KAIMU MKURUGENZI MPYA 

Bw. Fred Luvanda Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIB Corporate Bank Ltd (TIB CBL)

Benki ya  biashara inayomilikiwa na Serikali TIB Corporate Bank Ltd (TIB CBL) yenye matawi 7 kwa sasa ambayo ni Dar es salaam (3), Mwanza , Arusha, Mbeya na Dodoma huo imemteua Bw. Fred Luvanda kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji mpya. Uteuzi huo umekuja mara baada ya kuchukua uamuzi wa kusitisha uteuzi wa Bw. Frank Nyabundege kuanzia tarehe 13 Julai 2019.  Uamuzi huo umechukuliwa kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 33(1) na 33(2)(f)  pamoja na 33 (2)(b)cha sheria ya Mabenki na Taasisi za fedha ya mwaka 2006.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo mchana, Fred Luvanda ambaye ndiye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji mpya aliomba kutolewa taarifa sahihi kuwa Benki ya TIB Corporate haiko chini ya usimamizi wa mabenki bali ni mabadiliko ya uongozi wa juu tu.              (Aliyeondolewa ni Mkurugenzi Mtendaji).  Benki ya TIB Corporate inaendelea kuhudumia wateja wake kama kawaida kwa ubora na ufanisi wa hali ya juu.

“Nachukua nafasi hii kuwatoa wasiwasi wateja na wadau wote wa benki ya Biashara TIB na wananchi kwa ujumla, wajue kuwa  huduma zinaendelea kama kawaida, pia mfahamu kuwa Serikali na Benki kuu inatambua umuhimu wa Benki hii hivyo itaendelea kutoa ushirikiano wa karibu ili kuhakikisha Benki  inazidi kuboresha huduma zake na kukua kwa maendeleo ya nchi yetu. “Niwaombe menejimenti pamoja na wafanyakazi wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha benki inatimiza malengo yake,” alisema Luvanda.

Imeandaliwa na Neema Adrian na Stella Kasabo/GPL


Loading...

Toa comment