The House of Favourite Newspapers

Benki Ya NBC Yazindua Huduma Ya NBC Connect Kanda Ya Ziwa

0
Mkuu wa Kitengo cha Kidigitali na Miamala wa benki ya NBC Jimmy Myalize, akiwasilisha mada ya namna ya kufanya miamala kwa njia nafuu na rahisi wakati wa uzinduzi huduma ya NBC Connect kwa kanda ya Ziwa, katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza.

Mwanza Mei 19, 2023: Makampuni pamoja na taasisi mbalimbali ambazo ni wateja wa Benki ya Taifa ya Biashara ya (NBC), sasa wanaweza kupata uzoefu mpya wa huduma za kibenki kupitia huduma ya NBC Connect, ikiwa ni ingizo jipya la huduma za kibunifu za kidigitali.

NBC Connect, ni huduma ya kisasa ya kidigitali, ambayo huwezesha huduma salama za kibenki ambazo huweza kufanyika sehemu yoyote, muda wowote kwa njia ya mtandao. Huduma hii ni sehemu ya mchango wa benki katika kuunga mkono jitihada za serikali za kuongeza ujumuifu katika huduma za kifedha (financial inclusion).

Wilson Nkuzi Mkuu wa kwa Kitengo cha Wateja wa Kimataifa wa NBC Wilson Nkuzi, akizungumza na wateja wakati wa uzinduzi wa huduma ya NBC Connect kwa kanda ya Ziwa, katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza.

Uzinduzi wa huduma ya NBC Connect Kanda ya Ziwa, ni wa pili baada ya uzinduzi kwa kanda ya nyanda za juu kusini uliofanyika jijini Mbeya mwezi uliopita.

Kupitia NBC Connect, wateja wenye makampuni na taasisi mbalimbali zilizopo mkoa wa Mwanza na maeneo ya jirani, watapata fursa na uwezo wa kufanya miamala yao ya kifedha kwa urahisi zaidi na kupata uzoefu mpya katika kupata huduma za kibenki.

Huduma itawapa wateja uwezo wa kufanya miamala kirahisi ikiwa ni pamoja na malipo ya ndani na nje ya nchi, malipo ya serikali pamoja na malipo kwa mkupuo bila kuchukua muda kwa kutumia simu au kompyuta.

Baadhi ya wateja wa benki ya NBC na wadau wa sekta ya fedha wakipiga makofi kuipongeza benki hiyo, wakati wa kuzindua huduma ya NBC Connect kwa kanda ya Ziwa, katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza.

Wateja pia wataweza kupata taarifa za miamala waliyofanya popote pale walipo pasipo kulazimika kwenda benki.

NBC Connect imetengenezwa kwa teknalojia ya kisasa na yenye usalama wa hali ya juu ambayo imezingatia na kutoa kipaumbele kwenye usiri wa taarifa za mteja. Ubunifu wa huduma hiyo huakikisha taarifa za kifedha za wateja zinalindwa wakati wote.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bulandya Elikana, akizungumza na wateja wa benki ya NBC wakati wa kuzindua huduma ya NBC Connect kwa kanda ya Ziwa, katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo, mkuu wa kitengo cha wateja wa kimataifa wa benki ya NBC Wilson Nkuzi, “Tunafuraha kutambulisha NBC Connect kwa wakazi wa kanda ya ziwa na maeneo ya jirani.

Mfumo huu wa kibenki wa kidigitali ni uthibitisho wa dhamira ya kuwapatia wateja wetu huduma bora za kibenki ambazo ni rahisi, salama na zinazofaa na kukidhi mahitaji ya wateja.

NBC Connect itawawezesha wateja wetu kufanya huduma za kibenki popote pale, wakati wowote, na kufurahia huduma hizo bila matatizo.”

Pamoja na huduma rahisi na za kisasa, NBC Connect itatoa usaidizi wa binafsi kwa wateja kupitia kituo chake cha huduma kwa wateja ambapo mameneja wetu katika kituo cha huduma kwa wateja wanapatikana ili kuwasaidia wateja kulingana na mahitaji yao na kutoa mwongozo wa jinsi ya kutumia jukwaa hilo kwa ufanisi.

Ili kusherehekea uzinduzi wa huduma hiyo jijni Mwanza, Benki ya NBC itatoa maelezo ya kina juu ya huduma hiyo na kwa wateja watakaojiandikisha na kujiunga na huduma hiyo ili kuwapa uelewa mpana wa namna ya kuitumia na kufurahia huduma hiyo.

“Tunawaalika wateja wetu wote wa kanda ya Ziwa na maeneo ya jirani wajionee urahisi na usalama wa NBC Connect.

Ni huduma ambayo inaleta mapinduzi mapya katika namna ambavyo huduma za kibenki zinatolewa. Tuna uhakika kuwa wateja wetu watafaidika nayo kwa kiasi kikubwa, “aliongeza.

Kwa upande wake katibu tawala wa mkoa wa Mwanza Bulandya Elikana aliishukuru Benki ya NBC kwa ubunifu wao mzuri na kuwahimiza wateja kutumia mfumo huo mpya wa kibenki ili kurahisisha shughuli zao za kila siku.

“Uzinduziwa NBC Connect kanda ya Ziwa unawakilisha mpango mkakati wa upanuzi wa benki ya NBC ili kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.

Benkiya NBC inasifika kwa dhamira yake kubwa ya kuwajibika kwa jamii, ikiwa ni pamoja na kusaidia jamii kupitia mipango mbalimbali, kama vile Mbio za Kimataifa za NBC Dodoma Marathon zinazohamasisha matibabu ya saratani ya shingo ya kizazi, msaada wa afya ya uzazi kupitia kliniki zinazotembea, program za elimu ya kifedha, uwezeshaji wa vijana.

Kupitia udhamini wa Ligi Kuuya NBC, hakika napongeza juhudi hizi zinazofanywa na NBC” alisema.

Kuhusu Benki ya NBC:

Benki ya NBC ni taasisi ya kifedha inayoongoza nchini Tanzania inayotoa bidhaa na huduma mbalimbali za kibenki kwa watu binafsi, wafanyabiashara na jamii. Kwa kujitolea kwa dhati kwenye suala la huduma kwa wateja, uvumbuzi na uwajibikaji wa kijamii, NBC Connect inalenga kuwa mshirika wa benki anayeaminika kwa watu binafsi na biashara Tanzania nzima.

Leave A Reply