BETHDEI YA MAMA DIAMOND, TANASHA USIPIME – PICHAZ + VIDEO

USIKU wa kuamkia leo mama wa msanii wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond Platniumz’, Sandra Kasim na mpenzi wake Tanasha ‘Donna’ walisherehekea siku yao ya kuzaliwa  iliyoangushwa ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, Dar.

 

Hafla hiyo iliyoongozwa na wasanii wa lebo ya Wasafi Classic Baby (WBC) ilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo mastaa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, ambaye ni mlezi wa kundi hilo.

 

Katika shamrashamra hizo pia Diamond alitumia nafasi hiyo kuutambulisha ujauzito wa mpenzi wake, Tanasha, ambapo alisema una miezi saba kwa sasa.

 

Miongoni mwa matukio ya burudani yaliyojiri kwenye tukio hilo ni kuiunganisha familia ya msanii huyo ambapo pamoja na uwepo wa mama yake mzazi na mumewe Shamte pia baba wa mzazi wa msanii huyo, Abdul Juma, naye alifika na mpenzi wake Neema Isote.

 

Baada ya pati hiyo Diamond alimzawadia mama yake gari aina ya Land Cruiser V8 na mpenzi  wake alimzawadia Land Cruiser TX.

 

 

 

 

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL

Mama DANGOTE Na TANASHA Walivyokata KEKI Kwenye PARTY Yao..!


Loading...

Toa comment