Bethidei ya Amber Lulu… Pombe + Mahaba Vyatikisa

Mambo ni moto! Msanii wa Bongo Fleva, Lulu Eugen ‘Amber Lulu’, usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita alifanya sherehe ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa ‘bethidei’ ambapo pombe, mahaba vilitikisa.

 

Sherehe hiyo ya aina yake ilifanyika kwenye Ukumbi wa China Bar, Mbezi-Bondeni jijini Dar ambapo msanii huyo alitumia nafasi hiyo kumtambulisha mpenzi wake mpya aliyemtaja kwa jina moja la Sam ambapo alisema hataki kumuweka wazi sana kwa ajili ya kuwaogopa vidowezi wa mjini.

 

 

“Jamani huyu ndiyo naniliu wangu, yeye ni mkurugenzi f’lani hapa mjini, lakini sitaki kumpamba sana kwenye pati yangu hii nisije nikaibiwa bure na vidaka tonge wa mjini, naomba kwa leo mjue hivyo tu,” alisema Amber Lulu.

 

Katika sherehe hiyo pombe zilitawala kwani wageni waalikwa walikunywa kwa kadiri walivyojisikia ambapo kila mmoja alikolea kwa kilevi na hapo ndipo walipoanza kuonyeshana mahaba kila mtu na wake.

 

 

Amber Lulu alionekana kuwa na vituko kibao kwani alivaa kigauni kifupi chenye mpasuo mkubwa unaokaribia kufika kiunoni ambao uliwashangaza wengi na muungwana akiuona lazima ateme mate chini kuashiria kufuru.

 

Mambo yalikuwa ni moto zaidi baada ya kuwadia wakati wa kukata keki ambapo Amber Lulu alionesha mahaba niue kwa kumlisha mpenzi wake keki na kugandana naye kwa dakika kadhaa hivyo kusababisha wapenda ubuyu kuanza kuongea yao kila mmoja akisema lake.

 

Sambamba na hayo, baada ya tukio la kulishana keki, Amber Lulu alianza kumbanjukia mpenzi wake huyo kihasara na watu kubaki macho kodo.

 

Shamrashara zilizidi zaidi wakati wa kucheza muziki kwa sababu kila mmoja alikuwa akibanjuka na mpenzi wake kihasarahasara hadi usiku mnene kabla ya Ijumaa Wikienda kufungasha virago ukumbini hapo.

STORI: Richard Bukos, IJUMAA WIKIENDA | DAR ES SALAAM

Mambosasa: Abdul Nondo Alikwenda Iringa kwa Mpenzi Wake